Agizo la Makamu wa Rais wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuhakikisha
kanda yake inatokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Mama Samia ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo.
“Bado
takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha ukatili wa kijinsia unaendelea.
Kamanda Mambosasa tunakuachia wewe suala hili, likitokea tunakubana wewe
na wewe utawabana wenzako,” alisema.
Mama
Samia alisema serikali inaendelea kutekeleza Mpango mkakati wake wa
miaka mitano wa kutokomeza ukatili wa jinsia ili kuhakikisha ifikapo
mwaka 2020 ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unapungua kwa
asilimia 50.
“Bila
wanawake kuzitumia sera na sheria za wanawake na jinsia zilizotungwa na
serikali hatutafanya lolote. Isipokuwa tutazifungia na kuziweka katika
makabati na hatutafika kokote,” alisema.
Hata hivyo, Mama Samia alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwakomboa wanawake ikiwemo kufufua Benki ya Maendeleo ya Wanawake nchini (TWB).
“Serikali imechukua hatua mbalimbali kumkomboa mwanamke kiuchumi ili aweze kusaidia jitihada za serikali za kuleta maendeleo. Tuna Mpango wa kufufua benki ya wanawake, ni wajibu wenu kuhakikisha haifi. Watu wenye uwezo waisaidie serikali kuitafutia mitaji,” alisema.

Aidha,
Mama Samia aliwataka wanaume kutowanyanyasa wanawake kwa kuachana na
mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na jinsia.