WAZIRI APOKEA MRADI WA NYUMBA ZA SH 1.4 BILIONI
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe kushoto,Balozi wa Ujermani nchini Tanzania Dk Detlef Wachter katikati na Afisa Ujilani Mwema shirika la Frankfurt Zoological Society Masengeri Tumbuyo kulia wakikata utepe kama ishara ya kuzindua nyumba nne za watumishi na ofisi tatu za watumishi wa Idara ya Ujilani Mwema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilizojengwa kwa Ufadhili wa Serikali ya Ujermani kupitia Benki ya Maendeleo ya nchi hiyo KFW kwa thamani ya sh 1.4 bil,lengo likuwa ni kuhakikisha watumishi wengi wanahamia Fort Ikoma ambako ni nje ya ili kulinda na kuhifadhi Mfumo wa Ikolojia ndani ya Hifadhi hiyo.
Meneja Mahusiano wa Tanapa (mc)wa shughuli hiyo Paskael Shelutete
akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la Msingi mara baada ya
Waziri na Balozi kukabidhiana nyumba hizo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akipokea funguo
za nyumba nne na ofisi tatu toka kwa Balozi wa Ujermani hapa nchini Dk
Detlef Watchter zilizjengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujermani kwa
thamani ya sh 1.4 bilioni kwa ajili ya wafanyakazi wa Idara ya Ujilani
Mwema hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Waziri akiangalia mashine aina ya Hydroform ambayo wanaitumia kufyatua matofali ya gharama nafuu na ambayo hayachomwi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira,mashine hiyo ina uwezo wa kufyatua matofali 3000 kwa siku,inatumia mafuta ya dezeli lita 10 kwa siku.
Wakiangalia matofali yaliyokwisha fyatuliwa
Waziri Maghembe akimakbidhi funguo za nyumba nne na ofisi tatu Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Ujermani hapa Nchini.
Burudani kutoka kikundi cha COCOBA Bonchugu ilikonga nyoyo za watu
Waziri akikagua nyumba na ofisi kabla ya kuzindua
Moja ya nyumba ya watumishi iliyokabidhiwa
Wasomee jiwe limeandikwaje?
Mc Shelutete akifanya yake
Wanafuatilia taarifa kutoka kwa viongozi mbalimbali
Asante sana kwa msaada wa nyumba tunaomba mkamilishe mpango wa maji kutoka Borogonja na kituo cha Taarifa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti anasikika akisema Waziri
Picha mbalimbali za pamoja zilipigwa
Walizungukia maeneo