TIGO YACHIMBA KISIMA CHENYE THAMANI YA 18M/- KIJIJI CHA USONGELANI TABORA
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akipampu maji kuzindua
kisima cha maji alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo chenye thamani ya
18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana .
Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya ziwa (mwenye miwani), Alli
Maswanya, Diwani wa viti maalum kata ya Usoke, Aneth Msangama na Diwani
wa Usoke, Said Kazimilo.
Awali Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akifungua pazia
kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji kilichokabidhiwa na kampuni ya
Tigo chenye thamani ya Tsh 18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya
Urambo mkoani Tabora jana
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji
mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo, Nusura Swalehe mara baada ya
uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa
na kampuni ya Tigo kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani
Tabora jana .
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji
mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo, Rehema Maganga mara baada ya
uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa
na kampuni ya Tigo kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani
Tabora jana.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry akicheza mziki na baadhi ya
wakazi wa kijiji cha Usongelani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
kisima cha maji kilichotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi
nchini Tigo. Ni sehemu ya msaada wa Tigo katika kuhakikisha upatikanaji
wa maji safi na salama
*****
Tabora, Agosti 22, 2017- Tigo Tanzania imejenga kisima cha maji chenye
thamani ya Sh 18m/-katika kijiji cha Usongelani katika wilaya ya
Urambo, mkoani Tabora kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na kampuni hiyo
ya kuunga mkono ya kuunga mkono ustawi wa kijamii katika maeneo
inamohudimia pamoja na juhudi za kuunga mkono katika kuhakikisha kuwa
wananchi wote nchini wanapata maji safi na salama.
Akizungumza kwenye sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji
cha Usongelani mkoani Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally
Maswanya alielezea matumaini yake kuwa kisima hicho kitachangia kwa
kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo
kwa kuipatia jumuia ya eneo hilo kupata maji ya uhakika, safi na
salama.
"Tumejitahidi kuboresha maisha ya jamii , sio tu kwa kuhakikisha kuwa
wanafurahia huduma nzuri za mawasiliano kutoka katika mtandao wetu, bali
pia kupiga hatua zaidi kuhakikisha kuwa afya zao na ustawi wao
unaboreka," alisema.
Maswanya alibainisha kwamba msaada huo unafanya vijiji vilivyonufaika
kufikia 21, na hivyo kuwafanya watu zaidi ya 187,000 kunufaika na
kujituma huko kwa Tigo katika kuwapatia watu maji safi na salama kote
nchini.
Mwaka huu, Tigo inakusudia kuchimba visima katika maeneo yaliyo na
uhitaji mkubwa ambapo inatarajiwa kuwa zaidi ya watu 350,000
watafaidika na mchango wetu wa kuisaidia juhudi za za kupunguza uhaba wa
maji safi na salama uliopo nchini.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa
Aggrey Mwanri ambaye wakati akiwashukuru Tigo kwa msaada unaohitajika
sana alisema kuwa kisima hicho kitasaidia kwa kiwango kikubwa
kuimarisha afya na ustawi wa jamii kwa kusaidia kukua kiuchumi na
kijamii. Aliwataka watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza kuunga
mkono jitihada za kuondokana na tatizo la uhaba wa maji katika mkoa huo.
Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutusaidia katika jitihada zetu za
kuwapatia maji ya uhakika katika eneo hili kwa kutatua uhaba wa maji
uliokuwepo. Tunaamini kuwa upatikanaji wa maji safi na salama karibu na
makazi kutaongeza pia uzalishaji wa kiuchumi hasa kwa wasichana na
wanawake ambao hawatakuwa wakitumia tena muda mwingi kutafuta maji
safi mahali pengine. Hii itawapa wasichana fursa ya kuhudhuria kwa uhuru
shuleni na kuwapunguzia mzigo wa kijamii hasa wanawake, hivyo kupata
nafasi ya kushughulikia kwa ufanisi majukumu yao ya kila siku kwa
maendeleo ya taifa, " alisema Mkuu wa Mkoa.