Serikali Yakichukua kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries, Mwanza
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekichukua kiwanda cha kusindika
ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo eneo la viwanda Ilemela mkaoni
Mwanza kutokana na kushindwa kuendelezwa na wamiliki wake toka mwaka
1998.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza John Mongella ameamuru makampuni ya Skysraper na Caspian
kurudisha funguo za kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries Limited Mwanza
kwa Serikali na kuwa mali ya Serikali rasmi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ametangaza uamuzi huo kutokana na
wawekezaji wa kiwanda hicho kushindwa kukuendeleza lakini pia kuwepo kwa
udanganyifu wa umiliki wa kiwanda hicho uliodaiwa kufanya na kampuni ya
Quality Group.
Mongella
ametangaza maamuzi hayo mbele ya Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
ya mkoa huo, wakiwemo pia wawakilishi wa kampuni ya Caspian na Quality
Group zilizoshindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa kukiendeleza
kiwanda hicho toka mwaka 1998.