WADAU WAJADILI MASWALA YA KUMKOMBOA MWANAMKE KISIASA NA KIUCHUMI.
Mkurugenzi
wa Women Fund Tanzania Bi. Marry Lusimbi akitoa neno la utangulizi na
kuwashukuru wanawake viongozi wote waliojumuika kwa pamoja katika
Futari,na kujadili mambo ya msingi hasa ukombozi wa Mwaamke katika
maendeleo,kisiasa,kiuchumi na jamii inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.
Dr.
Eve Maria Semakafu,(wa katikati) akichangia jambo juu ya namna ya
wanawake viongozi wanavyoweza kusaidia katika kuhakikisha wanafunzi wa
kizazi cha sasa wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata elimu iliyobora
na kubadili mfumo wa ufundishwaji kwani kwa sasa inaonekana wamekuwa
wakidumaa sana kwa sababu ya kurahisishiwa kila kitu.
Blog za Mikoa
Blog za Mikoa
Bi.
Fortunata Manyeresa(wa kwanza kushoto) akieleza namna mbalimbali za
kuwafikia wanawake ikiwa ni pamoja na njia ya Vikoba,pia alielezea namna
wanavyofanya kazi kupitia Asasi yao ya kiraia ya Tree of Hope yenye
makazi yake Tanga
Bi.
Eluka Kibona kutoka Oxfam Tanzania akielezea kwa undani maswala ya
Siasa za ndani majumbani ambapo maana yake ni majukumu ya wanawake
katika kulea familia zao majumbani bila malipo na kuongeza kuwa hayo
yote yana mahusiano ya karibu baina ya matokeo ya uzoefu wa maisha ya
wanawake na mfumo wa nchi ikiwa ni pamoja na Sera pia siasa.
Mmoja
wa Viongozi wanawake Profesa Ruth Meena akieleza namna wanawake na
wasichana wanavyopoteza muda mwingi katika kufanya kazi ambazo hazina
malipo na kuwanyima kufanya kazi ambazo zingeweza kuwapatia kipato,
alisema kupitia mkutano huu kunapaswa kuwa na maadhimio ambayo
yatamsaidia mwanamke kuwa licha ya kufanya kazi za ndani lakini pia
apate muda na wakufanya shughuli ambazo zitamsaidia kuingiza kipato
Mkurugezi
Mtendaji wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania Bi. Tike Mwambipile
(Kulia) akichangia jambo wakati wa Futari hiyo ambapo alisema kuwa
ushirikishwaji wa wanawake vijana katika ukombozi wa mwanamke katika
kuleta maendeleo ni muhimu kwa kuwa wananguvu na wanatakiwa mwongozo
bora na kuwasaidia katika mambo mengine ili waje kuja kuwa viongozi bora
wa Baadae.
Happiness
Maruchu kutoka TGNP Mtandao ambaye alijikita katika nafasi ya vijana
katika kuhakikisha kwamba ukombozi wa wanawake kimapinduzi unakuwa
ajenda kuu ya kitaifa huku usawa wa kijinsia ukiwa nguzo ya kufanikisha
maswala hayo,na kuongeza kuwa wanawake vijana wanaweza kufanya mambo
makubwa ya kuwakomboa wanawake wengi zaidi.
Irene
Kiria kutoka HAWA akichangia jambo na kuwashukuru viongozi wote ambao
walifika katika Futari kwa kuwa amejifunza mengi na ataenda kuyafanyia
kazi zaidi katika kazi zake na aliongeza kuwa vyombo vya Habari ni
muhimu sana katika kufikisha taarifa hizi juu ya ukombozi wa wanawake.
Bi. Jane Remme Kutoka Asasi ya kimataifa ya kiraia Oxfam akichangia jambo wakati wa jukwaa hilo.
Mkurugezi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bw. Francis Odokorachi
(kulia) akizungumza na baadhi ya waliofika katika futari.
Kikao kikiendelea.
Asasi za Kiraia za Women Fund
Tanzania,HAWA,TGNP Mtandao na Oxfam Tanzania wamewakutanisha wanawake
viongozi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ili kujadili namna ya
ukombozi kwa wanawake ikiwa ni kisiasa,kijamii na kiuchumi na kuhaki kisha hiyo
ndio inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.
Akizungumza kwa niaba ya Asasi
zilizo andaa futari hiyo ya pamoja Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania Bi. Mary Lusimbi alisema kuwa mjadala huo
ulilenga kuwajenga viongozi hao kwenye mahusiano na ushirikiano wa wanawake
kufungua nafasi kwa viongozi wanawake wengine kushiriki pamoja ili kuleta
uwiano kijinsia .
"Tunaposema Masuala ya
Siasa za Ndani Majumbani tunaongelea majukumu ya Wanawake
katika kulea familia na nyumba bila malipo ukiwa na maana pana pia
ni kwamba kuna mahusiano ya karibu baina ya matokeo na uzoefu wa maisha
ya wanawake na mfumo wa nchi, sera, na siasa.," alisema
Wakati wa mjadala huo mpana wanawake
hao viongozi waligusia kwa kina kuwa nguvu ya malengo ya ukombozi wa
mwanamke kisiasa, kijamii na kiuchumi
itasukumwa kwa pamoja kutokana na umoja wa wanawake waliopo katika nafasi za
uongozi kupitia nafasi zao binafsi,taasisi na taaluma zao.
Walisema kuwa katika jamii zetu
kuna mila na desturi ambazo zinahusiana na jinsia zinazo onesha kwamba katika
jamii nyingi wanawake na wasichana hufanya kazi za nyumbani za kuhudumia
familia na kulea kwa muda mrefu zaidi kulipo wanaume kazi hizo ni pamoja na
kutunza wazee pamoja , kulea watoto, kuhudumia wagonjwa, kuandaa chakula,
kusafisha, kuchota maji na kukusanya nishati kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani, na kuongeza kuwa Takwimu zinaonesha kwamba pato la taifa lingeweza
kukuwa kati ya asilimia 10 hadi 39 endapo Serikali ingewekeza katika kazi za
nyumbani zisizo na malipo.
Pia ili kufanikisha haya Makundi
mbalimbali, Wadau na Serikali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ambayo ni pamoja na Kupunguza kazi za nyumbani
zisizo na malipo kwa kuweka mifumo sahihi itakayo rahisisha na kupunguza muda, Kuzitambua
kwa kuziweka katika mifumo ya kisera na kibajeti na pamoja na Kuhakikisha
makundi mbalimbali ya wanawake na wasichana yanapata uwakilishi katika
ngazi za maamuzi, Kugawanya kazi hizi kwa makundi tofauti na kwa
uwiano unaofaa kati ya wanawake na wanaume, jamii na familia.