SPORTPESA WAMLETA BOSI WA EVERTON, YUKO NCHINI, DK MWAKYEMBE AMPOKEA NA KUMUONEYSHA VIPAJI VYA VIJANA
DK MWAKYEMBE (KATIKATI) AKIJADILI JAMBO NA ELSTONE WAKATI WAKIWA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO. |
Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Everton, Robert Elstone yuko nchini.
Ugeni
wa Elstone umeratibiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa na mgeni
rasmi amekuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk
Harrison Mwakyembe.
Elstone,
ameongozana na nahodha wa zamani wa Everton, Leon Osman ikiwa ni hatua
moja kukaribia ujio wa Everton ambayo itakuja kucheza nchini mwezi ujao.
Uwanjani hapo pia alikuwepo Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.
Bosi
huyo wa Everton amepata nafasi ya kuwaona watoto na vijana wa
Kitanzania wakicheza soka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
leo.
Pia anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali ya maendeleo ya michezo.