KOTEI WA SIMBA APATA NAFASI YA "KUMUUMA SIKIO" MCHEZAJI GWIJI WA EVERTON
Kiungo kiraka wa Simba, James Kotei, amepata nafasi ya kubadilishana mawazo na nahodha wa zamani wa Everton, Leon Osman.
Osman yuko nchini katika ziara iliyoandaliwa na kampuni ya SportPesa hapa nchini.
Kotei na Osman wamekutana wakati ya hafla fupi ya kushuhudia vijana wenye vipaji wa Kitanzania.
Kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Osman amepata nafasi ya kuona
baadhi ya wachezaji wenye vipaji ambao walialikwa na kucheza na mpira.
Kati
ya watu waliokuwepo uwanjani ni mgeni rasmi Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia Ofisa Mtendaji
Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.
Osman
aliichezea Everton katika Ligi Kuu England na michuano mingine tokea
mwaka 2000 hadi 2016 alipotangaza kustaafu akiwa mmoja wa manahodha.