Picha: SHUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI KUJADILI MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
June 1,2017 Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga
(SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya Mkataba
wa Huduma Kwa Wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza
kutumika kuanzia Julai Mosi ,2017.
Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika katika ukumbi
wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Akizungumza katika warsha hiyo,Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili
rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo
yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa
watumiaji wa majumbani.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya alisema
kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na
wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.
“Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya
mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji
kwa wateja wetu”,alieleza Marco
Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa
ya Shinyanga,madiwani,viongozi wa dini,viongozi wa taasisi
mbalimbali,watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,waandishi wa
habari na wadau mbalimbali.
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA WARSHA HIYO
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza wakati wa
kufungua warsha/kikao cha kujadili rasmu ya huduma kwa wateja
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha
hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla,kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akizungumza katika warsha ya wadau wa maji manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akisisitiza jambo katika warsha hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya akielezea umuhimu
wa wadau wa maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akizungumza ukumbini
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza katika warsha hiyo
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akiendelea kuelezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja
Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe akifafanua kuhusu mktaba wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapole akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo
Warsha inaendelea
Warsha inaendelea
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akichangia hoja katika warsha hiyo
Diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini,Zenna Gulam (Chadema) akichangia hoja
Mchungaji Obeid Jilala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga (Chadema) akichangia hoja ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Warsha inaendelea
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog