Picha: MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MOSHI MSIBA WA NDESAMBURO,VIONGOZI WA CHADEEMA WAKIPOKEA MWILI WA MAREHEMU
Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa wameupokea
mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon
Ndesamburo baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo.
Ndesamburo alifariki ghafla wiki iliyopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi
Mjinim,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa kumi jioni utapelekwa
nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama
hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya
kumuaga Ndesamburo.
Matukio mbalimbali kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye msiba wa
Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki hivi karibuni mkoani humo,
Marehemu Ndesamburo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa
Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini utaagwa kwenye uwanja wa
Majengo kuanzia leo na kesho na kisha kuzikwa mkoani humo haya ni
matukio kadhaa ya picha za matukio yanayoendelea katika msiba huo.
Baadhi ya wa vijana waendesha bodaboda wakijiandaa kwa ajili ya
maandamano maalum wakati mwili wa marehemu utakapokuwa akipelekwa kwenye
uwanja wa Majengo.
Gari Maalum litakalochukua mwili wake.
Eneo la Uwanja wa Majengo ambalo ndipo shughuli za kuaga mwili zitafanyika likiwa limepambwa tayari kwa shughuli hizo.