Lowassa aeleza sababu za kutokuvaa sare za CHADEMA

"Si kweli kuwa sivai sare cha CHADEMA, hata nilipokuwa CCM nilikuwa nashona shati la rangi moja ama kijani au njano kisha naweka nembo maalumu ya chama, vivyo hivyo hata CHADEMA naweka nembo maalum.

"Na jambo kubwa hapa ni kuwa, nisihukumiwe kwa kuvaa au kutokuvaa sare za CHADEMA lakini kwa matendo yangu."

Hayo ni maneno yaliyotolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa alipokuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo cha Azam Tv, Charles Hillary aliyetaka kujua kwanini havai sare za CHADEMA katika matukio mbalimbali kama ilivyokuwa CCM.

Lowassa alienda mbali na kusema kuwa, sare si jambo kubwa sana kwani mtu anaweza kuvaa sare na bado akawa si mmoja wenu. Unaweza kukuta mtu kavaa nguo za kijani lakini kiukweli moyoni si wa CCM

Aidha, Lowassa alisema, alipomaliza Chuo Kikuu alikwenda jeshini na kwa muda wote huo alikuwa akivaa magwanda, hivyo alishavaa vya kutosha, na umri wake kwa sasa si wa kuvaa tena.

Alipoulizwa kama uamuzi wa kutokuvaa sare ni mbinu ya mwaka 2020 aweze kupata kuungwa mkono na wanachama wa CCM na CHADEMA, alicheka kisha akasema kuwa, kama ni mbinu basi anaamini itafanyakazi.
Powered by Blogger.