MCHEZAJI WA EVERTON ALIYELETWA NA SPORTPESA, AONA VIPAJI VYA WATANZANIA


Nahodha wa zamani Everton, Leon Osman yuko nchini katika ziara fupi iliyoatibiwa na Kampuni ya SportPesa.

Leon ameongoza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Everton, Robert Elstone ambaye kitaaluma ni mhasibu.


Kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Osman amepata nafasi ya kuona baadhi ya wachezaji wenye vipaji ambao walialikwa na kucheza na mpira.


Kati ya watu waliokuwepo uwanjani ni mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Osman aliichezea Everton katika Ligi Kuu England na michuano mingine tokea mwaka 2000 hadi 2016 alipotangaza kustaafu akiwa mmoja wa manahodha.



Powered by Blogger.