|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea
mkoani Mwanza ambapo hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele
cha Siku ya Mazingira Duniani.
Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji
mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt
Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa
Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika
kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo
kijijini Butiama.
Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya
Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa
sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
|
|
|
|