CHADEMA Wazuiwa Kumuaga Mzee Ndesamburo Uwanja wa Mashujaa
Mbunge
wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama
vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon
Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa.
Hatua
hiyo inakuja ikiwa tayari maandalizi yameanza kufanywa katika Uwanja wa
Mashujaa kwa ajili ya kuuga mwili wa Ndesamburo lakini OCD Moshi
amezuia na kusema shughuli hiyo itafanyika Majengo badala ya Mashujaa
kuepuka kuzuia shughuli za kila siku.