ZIMBWE JR ANAAMINI HAWA NDIYO WALIOINYIMA SIMBA UBINGWA...
Ligi Kuu Bara, imefikia tamati juzi Jumamosi na Yanga kuibuka mabingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.
Hali
hiyo imemsononesha vilivyo beki wa kushoto ya Simba, Mohammed Zimbwe
maarufu kama ‘Tshabalala’ na kujikuta akisema kuwa African Lyon ndio
walioikosesha ubingwa Simba msimu huu.
Zimbwe
Jr amesema kuwa kitendo chao cha kukubali kufungwa na African Lyon
mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ndiyo sababu kubwa ya kukosa ubingwa.
Alisema kama wangeshinda mechi hiyo, leo hii wangekuwa wanasherehekea ubingwa wa ligi kuu baada ya kuukosa kwa muda mrefu.
“Nimeumia sana lakini hamna jinsi tujipange tu kwa ajili ya msimu ujao, msimu huu mambo yamekwenda ndivyo sivyo.
“Kilichosababisha
tukaukosa ubingwa huu binafsi naona ni kitendo chetu cha kukubali
kufungwa na Afican Lyon, hakika mechi hiyo iliniumiza sana, kwani hapo
ndipo tulipopoteana, kama tungeshinda mechi hiyo leo hii tungekuwa
tunashangilia,” alisema Zimbwe Jr.
SOURCE: CHAMPIONI