ABDULRAHMAN MUSA, MSUVA KILA MMOJA KULAMBA SH MILIONI TANO ZA USAJILI
MSUVA NA ABDULRAHMAN MUSA WAKIWANIA MPIRA KATIKA MOJA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA. |
Washambuliaji Abdulrahman Mussa wa Ruvu
Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye Ligi
Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.
Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara
kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14, watagawana zawadi ya
mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000.
Yanga imemaliza Ligi hiyo ikiwa bingwa
kwa ponti 68 na kufunga jumla ya mabao 57, wakati Ruvu Shooting
iliyomaliza katika nafasi ya saba kwa ponti 36 imepachika jumla ya mabao
28.
Watakabidhiwa zawadi hiyo katika hafla
ya tuzo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017
itakayofanyika keshokutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam.