WAZIRI WA KILIMO AZINDUA MWONGOZO WA KILIMO KINACHOHIMILI TABIANCHI.
Mathias Canal
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Dk. Charles J. Tizeba (MB) amezindua Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi. Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Wizara katika makao makuu mjini Dodoma.

Uzinduzi huo
umefanyika wakiwepo washiriki na wadau mbalimbali wa maendeleo
ikiongozwa na DK. Fred Kafeero, Mwakilishi Mkazi wa FAO, Dk. Sebastian
Grey, Mwakilishi wa CIAT.
Wengine
waliokuwepo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Maji na
Mazingira, Mheshimiwa Dk. Mary Nagu (MB), na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Atashasta
Nditiye (MB).
Washiriki
wengine walikuwa ni wadau wa kilimo hapa nchini kama vile taasisi zisizo
za kiserikali, sekta binafsi ambazo wanashirikiana na serikali katika
maendeleo ya kilimo hususan kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.