UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO.
Kaimu Katibu
Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward
Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam
jana Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo
wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam
Baadhi ya
wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo
kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es
salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam jana katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu
Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward
Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu
wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya
UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es
salaam
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa
Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es
salaam.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Maandalizi ya
ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule
za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba Moto katika Uwanja wa Uhuru na
Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es salaam.
Maandalizi hayo
kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya mkoa wa Dar es salaam
yalianza jana Mei 28, 2017 Kwa kuhusisha Manispaa za mkoa wa Dar es
salaam ikiwemo Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Kgamboni na Ubungo.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mashindano hayo kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es
salaam Kaimu Katibu Tawala katika upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa
Dar es salaam Ndg Edward Otieno aliwasihi washiriki kutumia weledi wao
wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili
kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.
Wanafunzi hao
ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31,
2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano
hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba June 6, 2017.
Otieno alisema
kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa
zaidi duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote Cha
mashindano.
Aliongeza kuwa
wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es salaam zitakwenda
Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki
pekee.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo aliyezuru
katika Uwanja wa Uhuru kujionea Timu ya Vijana wake kutoka Manispaa ya
Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala alipongeza juhudi
za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya Hali ya juu.
"Ukiona vijana
Wana nidhamu Kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana Bado
Wana safari ndefu kimichezo na kimaisha" Alisema MD Kayombo.
Mkurugenzi
Kayombo alitilia msisitizo zaidi kutumia weledi wao ili kurejesha
heshima ya michezo katika Manispaa ya Ubungo na Mkoa wa Dar es salaam
Kwa ujumla.