WANAHABARI, WATAFITI WA KILIMO KUTOKA NCHI TANO ZA AFRIKA WAAGANA JIJINI MWANZA.
Mwanahabari Lucy Ngowi (kushoto),
akichangamkia mapochopocho katika hafla ya kuagana kati ya wanahabari
kutoka nchi tano za Afrika na wataalamu wa kilimo kutoka katika nchi
hizo baada ya kumaliza ziara ya utoaji wa mafunzo kwa maofisa ugani wa
Wilaya ya Chato mkoani Geita na Buchosa Sengerema hafla iliyofanyika
Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana usiku. Mafunzo hayo
yaliandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana
na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima
Wadogo (AATF). Kutoka kulia ni Ofisa kutoka idara ya Fedha Tume ya Taifa
ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mr Nyamka na dereva wa Costech Mr.
Nasibu.
Mr. Nyamka na dereva Mr. Nasibu wakiwa katika makulaji wakati wa sherehe hiyo.
Hapa ni kujiachia kwa kwenda mbele.
Wanahabari kutoka Tanzania, Kenya,
Uganda, Ethiopia na Burknafaso wakiserebuka hapo wimbo kutoka Ethiopia
upkipigwa na huyo jamaa aliyeinua mikono juu kwa mzuka ni mwanahabari
kutoka Ethiopia akifurahia mziki wa kwao.
Hapa ni furaha tupu. Kushoto ni
mwanahabari kutoka Uganda na wapili kushoto ni mtaalamu wa kilimo na
mtafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia nchini Burknafaso, Dk. Traore.
Wanahabari na watafiti wakifurahi katika hafla hiyo.
Watafiti wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB),
Daniel Otunge, Mshauri Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi
Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania Dk.Alois Kulaya na
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk. Nicholaus
Nyange.
Mkuu wa Mradi wa
Utafiti wa Mahindi Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania
Dk.Alois Kulaya (kulia), akiongoza kusakata rhumba kwenye hafla hiyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi waa Habari za Kilimo
(TAJF), Gerald Kitabu.
Mserebuko ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Mwanza
WAANDISHI wa Habari na Watafiti wa
kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na
Tanzania wameagana katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza
jana baada ya kumaliza ziara ya utoaji wa mafunzo kwa maofisa Ugani wa
Mkoa wa Geita na Wilaya ya Buchosa Sengerema.
Hafla hiyo iliandaliwa na Jukwaa
la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti
na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF).
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na (OFAB)
kwa kushirikiana na (AATF) yalikuwa na lengo la kuwakutanisha
waandishi wa habari na wataalamu wa kilimo kutoka katika nchi hizo
waweze kukutana na kupeana uzoefu wa jinsi ya kuandika habari za kilimo
kwa kutumia Bioteknolojia.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu
wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema
mafunzo ya namna hiyo yataendelea kutolewa ili kuwajengea uwezo
wanahabari wanaoandika hababari za kilimo ili waweze kuandika habari
hizo kwa ufanisi bila kukiuka maadili.
"Tutaendelea kuwawezesha wanahabari
wanaoandika habari za kilimo ili wawe na uwezo wa kuandika habari za
kilimo kwa weredi mkubwa" alisema Nyinondi.