MISHAHARA JANGWANI YAFIKIA MIEZI MINNE, WACHEZAJI WALIA CHINICHINI
Bundi
wa maisha magumu ameendelea kuzunguka katika mitaa ya Jangwani baada ya
wachezaji wake kuanza kulalama chinichini kwamba mshahara sasa umefikia
miezi minne.
Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi minne sasa, jambo ambalo limewafanya waanze kulalamika.
"Kabla ya kwisha kwa ligi, tuliambiwa tupambane kubeba ubingwa. Mambo yatakuwa safi, lakini naona hali si nzuri hadi sasa.
"Mwisho
wa mwezi huu (Mei), itakuwa miezi minne. Mmekuwa mkisema hatujitumi,
hatuvumilii. Basi sasa mtutetee, maana miezi minne mingi ndugu zangu na
sisi tuna familia," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.
Viongozi
wa Yanga wamekuwa wakikubali kwamba mishahara imekuwa tabu na baada ya
kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji, mambo yamezidi kuwa mabaya
zaidi.
Wachezaji
hao walipambana mwishoni bila ya mishahara hadi kufanikiwa kufikisha
pointi 68 zilizowapa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.