WALIMU NA ASASI ZA KIRAIA WAJENGEWA UWEZO KUHAMASISHA UKUSANYAJI WA RASILIMALI ZA NDANI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU.
Afisa
Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akielezea juu ya
uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu kwenye
mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa
nchini mkutano huu umewakutanisha wanachama wa chama cha walimu
Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida.
Mkufunzi
wa Mafunzo, Wakili Dominic Nduguru akitoa mada ya uhusiano wa Makusanyo
ya Kodi Na Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa baadhi ya wadau na
mbalimbali wa elimu mkoani Singida leo kwenye mkutano ulioandaliwa na
TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja
Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akichangia mada
wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi
za Kiraia waliokutana mkoani Singida leo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe akielezea hali ya
elimu mkoani Singida na namna ambavyo uwekezaji wa Elimu ni muhimu
kuinua Sekta ya Elimu hapa nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo
Washiriki wakijadili juu ya upotevu wa kodi nchini kwenye mafunzo yaliyowakutanisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
Godfrey Adrof
Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.
Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.
Mkutano
huu ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa
nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za
walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu
wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike,
upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi
wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha
Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.
Mgawanyo
wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na
mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe.
Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa
fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali
mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa
mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa
wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.
Katika
majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani
katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za
kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini.
Akizungumza
leo Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia
Kamugisha aliwasisitiza serikali kuimarisha vyanzo vya mapato yetu kama
nchi hasa kwa kukusanya kodi stahiki kwa kila mtu anayepaswa kulipa
kodi. Ili tuondokane na utegemezi toka kwa wahisani. Kwa bajeti ya elimu
2016/17 takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa
kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. Hata hivyo
hadi kufikia mwezi Machi 2017 wahisani walikuwa wametoa kiasi cha
shilingi bilioni 132 tu, sawa na asilimia 47.6%.
Naye Mwenyekiti
wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe alisema ni vyema
serikali iimarishe vyanzo vyake vya mapato vya ndani, ili kuepuka aibu
hii, na pia walisisitizwa wadau wa elimu wanalo jukumu la kuisimamia
serikali katika kutimiza wajibu wake. Kila mtu akilipa kodi stahiki
kadri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu
wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika
makato hayo.