WAANDAAJI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA KUBURUZWA MAHAKAMANI
Kurugenzi ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP imekusudia
kuwasilisha kwa kampuni inayoandaa MISS TZ notisi ya madai na kusudio la
kuwafikisha Mahakamani kama watashindwa kuwalipa washindi wa MISS TZ
2016.
Hatua hiyo inakuja baada ya Kurugenzi hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa
mamiss walioshiriki Miss Tanzania 2016 na kushinda nafasi za 2, 3 na 4
kutolipwa fedha zao walizoahidiwa na waandaaji wa mashindano hayo Lino
International Agency Ltd.
TSNP imewataja washindi hao kuwa ni Mary Peter Clavery (Miss TZ 02),
Grace Christopher Malikita (Miss TZ 03) na Anna Nitwa (Miss TZ 04)
ambapo tayari mawakili wemepitia mikataba yao na kujiridhisha kuwa
waandaaji wamekiuka.