RAIS MAGUFULI AMUAPISHA SIMON SIRRO KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA
Rais John Magufuli amemuapisha mkuu mpya
wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua
nafasi ya Ernest Mangu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais,
Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba na makamishna
mbalimbali wa jeshi hilo.
Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.