TIKETI ZA SIMBA VS MBAO FC KOMBE LA SHIRIKISHO, ZAGEUKA ALMASI
Ule
mtanange wa Simba vs Mbao FC katika mechi ya fainali ya Kombe la
Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma umeokana kuwavuta watu
wengi sana.
Asilimia
kubwa ya mashabiki walikuwa wakihaha tokea jana wakitaka tiketi kwa
ajili ya kuingia uwanjani na zinaonekana kuwa adimu utafikiri madini ya
almasi.
Lakini hadi leo asubuhi, tiketi zinaonekana kuwa lulu kila mtu akitaka na imeelezwa wako walionunua nyingi na kuanza kulangua.