MASHABIKI WA SIMBA DODOMA WATUMA UJUMBE KWA MBAO FC
Mashabiki wengi wa Simba wameonekana kujiamini kwenda katika mechi ya fainali inayopigwa leo.
Simba
vs Mbao FC katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini Dodoma ndiyo mechi inasubiriwa zaidi hapa nchini na
mashabiki wa Simba wamekuwa wakiranda mitaani na mabango yenye ujumbe
tofauti.
Ujumbe
ulio katika mapango hayo unaonyesha mashabiki wa Simba wanajiamini kuwa
leo mwali ni wao na safari ya kushiriki michuano ya kimataifa,
imewadia.
Hata hivyo, watalazimika kusubiri dakika 90 za mechi hiyo ili kupata uhakika.