TFF YAITWANGA YANGA FAINI YA SH MILIONI MOJA, KISA?
Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na Yanga kugoma kuingia vyumbani.
Mechi namba 206 (Yanga 1 Vs Toto Africans 0).
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh.
1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati
wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 9, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa
Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu. Uamuzi huo umezingatia pia kuwa Yanga
imekuwa ikirudia kosa hilo mara kwa mara.