MAMBO YAMEKWIVAAA....RAIS FIFA AIPONGEZA YANGA KWA KUBEBA UBINGWA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino,
Mei 24, mwaka huu alituma ujumbe Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kuipongeza Young Africans ya Dar es Salaam kwa kutwaa ubingwa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
Young
Africans imetwaa Kombe hilo ikiwa ni mara tatu mfululizo na katika
salamu za pongezi, Rais Gianni Infantino amesema ubingwa huo wa Young
Africans ni kielelezo cha ushirikiano baina ya wachezaji, kocha,
utawala, matabibu pamoja na mashabiki.
Katika
pongezi zake Rais Infantino ameishukuru Young Africans na shirikisho la
mpira wa miguu la nchi kwa kusadia kupeleka ujumbe chanya kwa jamii
kuhusiana na mpira wa miguu.