TERRY AKABIDHIWA MKANDA WA MIELEKA WA WWE, NI HESHIMA KUTOKA WATU WA MIELEKA
John Terry anasubiri kuliinua Kombe la ubingwa Ligi Kuu England kwa mara ya mwisho, leo.
Lakini Shirikisho la Mieleka Dunia la WWE, limeonyesha heshima kwake kwa kumkabidhi mkanda maalum.
Mkanda
huo unafanana na ule anaoushikilia bingwa wa WWE, Randy Orton lakini
aliopewa Terry umepambwa na nembo za Chelsea kuonyesha heshima kwake
pamoja na klabu yake.
Huenda
Terry akawa na mkanda huo wakati wa kupokea kombe ambalo Chelsea
imelibeba msimu huu baada ya kufanya vibaya msimu uliopita chino ya Jose
Mourinho.