MOURINHO AMUINGIZA ZLATAN MAJINI KUHAKIKISHA ANACHEZA FAINALI EUROPA
Inaonekana Kocha Jose Mourinho ameanza kufanya juhudi kuhakikisha anampata mshambulizi Zlatan Ibrahimovic katika fainali ya Kombe la Europa dhidi ya Ajax.
Fainali
ya Europa itachezwa Mei 24 jijini Stockholm, Sweden ambako ni kwao
Zlatan na Ajax ni timu yake ya kwanza kubwa kucheza nje ya Sweden.
Zlatan
ambaye aliumia vibaya goti lake, tayari ameanza mazoezi maalum yakiwemo
yale ya ndani ya maji ili kuhakikishaa napona haraka.
Hivi karibuni, Zlatan alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pittsburgh na amekuwa akiendelea vizuri.
Juhudi hizo za sasa ni kujaribu kumpata ili kuwa na mtu wa uhakika.
Hivyo Zlatan amekatisha mapumziko yake ili kujaribu kurejea kwa kupitia matibabu hayo.