BAADA YA TAARIFA KWAMBA ANATAKA KUONDOKA, HIMID MAO AIBUA MAPYA SUALA LA BOCCO


Baada ya kusambaa kwa taarifa za nahodha wa Azam FC na mshambulizi tegemeo, John Bocco kuwa ametemwa Azam FC zimeenea kila sehemu mitandaoni, sasa yameibuka mapya.

Kiungo wa Azam FC, Himid Mao, naye ametupia mtandaoni taarifa ya kwamba akaunti ya Instagram ya Bocco imetekwa na wadukuzi wa mtandaoni.

Himid amesema kwamba kama kuna mtu anajua namna ya kurudisha akaunti kutoka kwa hao “hackers” basi atoe msaada.

Tayari watu mbalimbali wakiwemo wanasoma kama Juma Abdul, Thomas Ulimwengu na wengine wamekuwa wakitoa mawazo yao nini cha kufanya.


Hata hivyo, Himid hakueleza ni lini akaunti Bocco ilivamiwa kwa kuwa tokea Februari 13, inaonekana Bocco alianza kuweka maneno yanayoashiria kutokuwa na furaha au kama mtu aliyechoshwa na jambo na angependa aondoke zake.
Powered by Blogger.