Tani 16 za sukari ya Magendo
zimekutwa na jeshi la polisi kwenye ghala la afisa Mipango wa manispaa ya Musoma
John Masero katika kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba Wilayani hapa mkoani
Mara.
Kaimu kamanda wa mkoa wa polisi
Tarime/Rorya Sweetbert Njewike alisema watu 20 akiwepo afisa mipango wa
manisapaa ya Musoma wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukutwa wakifanya kazi
ya kubadilisha sukari kutoka kwenye mifuko yenye nembo ya kiwanda cha sukari
cha Kagera kwenda kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni ya Sonny Sugar ya Nchini
Kenya.
Meneja wa mamlaka ya
mapato mkoani Mara (TRA) Erenest Nkangaza alisema kuwa watu hao walikuwa
katika harakati za kubadilisha sukari ya tanzanikutoka kwenye mifuko yake na
kuika kwenye mifuko ya kiwanda cha Sukari cha Sonny cha nchini Kenya.
“wakati serikali ikiwa kwenye
upungufu mkubwa wa sukari ndipo watanzania wanafanya kuhujumu sukari ya viwanda
vyetu kupeleka Kenya ili kukwepa kodi, hili tunalifanyia kazi na tayari
tunawashirikilia watu 20 akiwemo mmiliki wa ghala hilo ambao baada ya uchunguzi
kukamilika sheria itafuata mkondo wake,”alisema Nkangaza.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo
yametokana na uchunguzi mzuri wa vyombo vya ulinzi uliofanyika katika eneo hilo
na kufanikiwa kutambua ghala hilo ambalo limekuwa likitumika kufanya uhujumu
huo kwa kukwepa kodi ili kujipatia faida nyingi.
“Baada ya kufika katika ghala hilo
tulifikili kuwa ni sukari ya kagera tu lakini kumbe kulikuwa na mifuko ya TPC
na Kilombero huu ni ushahidi tosha kuwa watu hawa wamekuwa wakifanya hivi kwa
muda mrefu na wajue kuwa biashara ya magendo haikubaliki, utaratibu ni mzuri tu
kupitisha bidhaa kwenye mpaka wetu wa sirari tunatoa huduma nzuri tunawaomba
wafanyabiashara waache,” alisema Nkangaza.
Kutokana na hali ya wafanya biashara
kutorosha shehena za bidhaa hasa sukari bei ya bidhaa hiyo imepanda kutoka sh,
2600 kwa mwezi wa tatu hadi sh, 3600 kwa kila huku mfuko wa kilogramu 25
ikiizwa kwa sh, 70,000 na 140,000 -145000 kwa mfuko wa kilogramu 50 katika
mpaka wa Sirari.
Aidha katika uchunguzi uliofanyika
na vyombo vya ulinzi umeonyesha kuwa zoezi la kubadilisha sukari kutoka kwenye
mifuko ya Viwanda vya serikali ya Tanzania kwenda kwenye viwanda vya nchi
jirani ya Kenya.
“Ushahidi unaonyesha kubwa kiasi
kikubwa kimekuwa kikitoroshwa kutokana na mazingira ambayo tumeyaona katika
hilo ghala jambo ambalo linazuia wananchi kupata bidhaa hii kwa
urahisi,”alisema Nkangaza.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Tarime Glorious Luoga amesema kuwa Serikali imejipanga vyema kwa lengo la
kutokomeza suala zima la magendo ili kuweza kukusanya mapato.
“Wafanyabiashara wafuate taratibu
zote katika mpaka wa sirari na siyo kufanya biashara ya Magendo” alisema Louga.
|