Timu
ya Taifa ya vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo
Jumatatu inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa
Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini
Gabon.
Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.
Akizungumza
kwa njia ya simu jana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime,
alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha
kuwakabili vijana wa Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.
“Kikosi
kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani
tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi
kutuombea,” alisema Bakari Shime.