Zacharia Hans Poppe, amereja Simba.
Uamuzi wa Hans Poppe kurejea Simba umetokana na mkutano uliofanyika hadi saa 9 usiku wa kuamkia leo.
Hans Poppe amethibitisha kurejea kwake kundini baada ya mkutano huo na viongozi.
Hans
Poppe aliamua kujiondoa katika kamati ya utendaji ya Simba na akawa
akawa ametoka kwenye kamati ya usajili aliyokuwa mwenyekiti.
Lakini kikao hicho hadi saa 9 alfajiri usiku wa kuamkia leo, kimemaliza suala hilo na Hans Poppe ameamua kurejea.
“Kweli
tumekutana hadi saa 9 usiku, mwisho tumekubaliana na tumeyamaliza
vizuri. Huu ni wakati wa kusonga mbele,” alisema Hans Poppe.