SERENGETI BOYS KUTUA NCHINI MCHANA SAA TISA KASORO
Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la
Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka jijini Libreville, Gabon saa 7.15
usiku wa kuamkia kesho Jumatano na itaingia saa 8.50 mchana ambako moja
kwa moja itakwenda kambini Hoteli ya Urban iliyoko katikati ya jiji la
Dar es Salaam, Tanzania. Watasafiri kwa ndege ya Afrika Kusini.
Alfred Lucas
MSEMAJI TFF