EXCLUSIVE: KAULI YA MANJI BAADA YA KUTANGAZA KUACHIA NGAZI YANGA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amethibitisha kuwa taarifa iliyoenea mitandaoni ni yake.
Manji amethibitisha kuandika barua ya kuanchia ngazi katika klabu ya Yanga kupitia nafasi yake ya uenyekiti.
“Kama ulivyoisoma hiyo taarifa, inajieleza kila kitu na mimi nisingependa kuongeza jambo zaidi.
“Kauli yangu ni ile katika taarifa niliyotoa. Nafikiri sitazungumza kitu kingine zaidi kwa sasa,” alisema.
Tayari mijadala mbalimbali imeanza kuzuka mitandaoni baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo ya Manji kujiuzulu.