News Alert !! WACHEZAJI WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI SINGIDA
Gari lililobeba wachezaji wa Ruvu Shooting likiwa limepata ajali
Habari tulizozipata hivi punde ni
kwamba msafara wa timu ya Ruvu Shooting umepata ajali mbele kidogo ya
Singida wakiwa safarini kurejea Dar es salaam.
Taarifa kutoka kwa mmoja wachezaji
waliokuwapo inasema kwamba gari likiwa katika mwendo tairi lilipasuka na
kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.
Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida.
Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde....