MWAMUZI WA TANGA APEWA MECHI YA FAINALI ASFC SIMBA v MBAO
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 13 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup HD
msimu wa 2016/17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua
Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Simba
SC na Mbao SC utakaofanyika Uwanja wa Jamburi Mei 27, 2017 kuanzia saa
10.00 jioni.
Kikumbo
atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati
mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha.
TFF
inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao
pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa
kila upande.
Alfred Lucas Mapunda
Ofisa Habari na Mawasiliano TFF