KASEKE, CHIRWA, MSUVA WASIMAMISHWA LIGI KUU BARA, MWAMUZI AONYWA
Kamati
ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni
kuhusiana na wachezaji wa Yanga kumuangusha mwamuzi wakati wa mechi yao
ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC na imewamua kuwasimamisha kuitumikia
Ligi Kuu BAra.
Wachezaji
Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa
kucheza mechi za Ligi Kuu wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na
kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Walifanya
kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20,
2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati
umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
Mwamuzi
Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi
dhidi yake ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti
wa Waamuzi.