MSICHANA AMKATA SEHEMU ZA SIRI MWALIMU WA DINI ALIYEMBAKA
Mwanamke mmoja nchini India amezikata sehemu ‘nyeti’ za mwalimu wa dini
katika jimbo la kusini la Keral kwa kudai kuwa alimbaka kwa miaka mingi.
Polisi wamesema kuwa mtuhumiwa anayejulikana kama Gangeshananda
Theerthapada alikuwa akizuru katika nyumba ya mwanamke huyo ili
kumfanyia matambiko ya ibada baba wa mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.
Mama yake alikuwa na matumaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyejidai kuwa
mtakatifu ataiondolea familia hiyo matatizo. Badala yake alikuwa
akimbaka msichana huyo mwenye miaka 23 kila anapotembea nyumba hiyo.
Ijumaa iliyopita alichukua kisu na kumshambulia alipojaribu kumbaka na
baadaye akaita maofisa wa polisi. Mbakaji huyo alikimbizwa hospitalini
ili kufanyiwa upasuaji wa dharura