Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles
Mlingwa amewahakikishia usalama waandishi wa habari Mko wa Mara na kuwataka
waendelee kufuata maadili, kanuni na Misingi ya habari ili kutekeleza vyema
majukumu yao.
Hayo yamebainishwa jana katika
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo ufanyika May tatu kila
mwaka na Mkoa wa Mara imefanyika jana katika ukumbi wa Mativilla Beech Mjini
Musoma na Mageni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Aidha Mkuu wa mkoa aliongeza kuwa
Wandishi wa habari mkoani mara wanapaswa sasa kuzitangaza fursa zilizpo mkoani
mara
Frida Mungulu ambae ni meneja wa Sido
Mara amewataka wandishi wa habari kuzitangaza fursa hizo ilikuweza kuyafikia
malengo na kuunga serikali katika uchumiwa viwanda.
Amesema bado kuna haja ya watumishi
mbalimbali wa serikali kwa kushirikiana na wandishi wa habari ili kuibua viwanda
vidogo na kuvitangaza ambavyo
havifahamiki hivyo kutumia taaluma yao
wandishi wanaweza kutangaza na hata kuboresha.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt
Vicent Naahano amesema kuwa kwa kutumia viwanda mpaka sasa ndio maana walizuia
kuwepo na uvuvi haramu ili kuendeleza viwanda vilivyopo Mkoa wa Mara.
Aidha Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Mara MRPC Jacob
Mugini amesisitiza waandishi kufuata Maadili ya Habari ikiwa ni pamoja na
kutumia vyema fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Mara.
|