MKULIMA MBARONI KWA KUTAPELIWA AKITUMIA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA -JWTZ
Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31)
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kufuatia kukutwa na sare
na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo
anatuhumiwa kuvitumia kupateli nakuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka
kwa vijana wanaotafuta nafasi yakujiunga na Jeshi hilo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa
alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya hatua
mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.
Alisema kuwa Polisi walifanikiwakumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli
ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na
kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.
Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za
likizo, fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye
nembo inayofanana na Jeshi hilo.
Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na
sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli
wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya
Kujenga Taifa na la Wananchi.
Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia
alikutwa na barua kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina
ya Toyota Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea
kuchunguza uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa
akilitumia na kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia
kupata nafasi katika majeshi.
Aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo na barua za maombi ya watu yakuomba
kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na
kalaya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.
Kufuatia tukio hilo alitoa witokwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na
nje ya Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze
kutoa ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na
mtuhumiwa huyo .
Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ
ili iweze kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na
ni nani aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo
vya Sheria kwa hatua zaidi.
Aidha, Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai
fedha na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani
vyombo hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana
wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wahiari na sio kwa kuchangishwa
fedha.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata
watuhimiwa 17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa
kukamata wa watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa
watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote. Aidha, alisema
kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na
nusu za mashamba ya zikiwana uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa
katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.
Alisema kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo
zinaendelea na kuwaomba wananchi wenye taarifa yawalipo wahusika
walisaidie Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama
kujibu tuhuma zao.