KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA AWATAKA WADAU WA SEKTA YA AFYA KUFANYA KAZI KWA UWAZI NA KUSHIRIKIANA
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga
Albert Msovela amewataka wadau wa sekta ya afya mkoani Shinyanga kufanya
kazi kwa ushirikiano,umoja na uwazi ili kuhakikisha changamoto zilizopo
katika sekta hiyo zinapungua kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Msovela ametoa rai hiyo leo wakati wa
kufunga kikao siku mbili cha wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga
kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzia May
30,2017 hadi May 31,2017 kilichokutanisha pamoja mashirika na taasisi
zaidi ya 30 zinazojishughulisha na masuala ya afya.
Msovela alisema serikali mkoa wa
Shinyanga inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika na taasisi
katika kushughulikia masuala ya afya hivyo kuwataka waungane pamoja
badala ya kila mmoja kufanya kazi peke yake ili kumaliza changamoto
zinazoikabili sekta hiyo.
Aidha Msovela alitoa wito kwa wadau wote
wa afya wanapoanza kutekeleza miradi mipya waripoti katika ngazi ya
mkoa na wilaya huku akiwasisitiza kuwasilisha mipango kazi yao sambamba
na kuwa wa wazi ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza.
ANGALIA HAPA PICHA ZA MATUKIO
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa kufunga kikao cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumzia kuhusu
umuhimu wa wadau wa afya kukutana na kujadili masuala ya afya katika
jamii
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza na wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga
Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko,Athanas Lucas akielezea kuhusu magonjwa
ya mlipuko ambapo aliitaka jamii kuchukua tahadhali juu ya magonjwa ya
mlipukovile Ebola,Surua na Rubella,polio,pepopunda ya watoto
wachanga,kipindupindu,homa ya uti wa mgongo na kichaa cha mbwa.
Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela na Mganga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume wakisikiliza kwa makini
mada kuhusu magonjwa ya mlipuko
Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko,Athanas Lucas akiendelea kutoa mada kuhusu magonjwa ya mlipuko
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE,John Myola akielezea kuhusu shughuli
zinazofanywa na shirika hilo katika kupiga vita vitendo vya ndoa na
mimba za utotoni
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini
Mratibu wa damu salama mkoa wa Shinyanga,Joel David akielezea kuhusu
mahitaji ya damu mkoa wa Shinyanga ambapo aliomba wadau waendelee
kujitokeza kutoa damu ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa damu
katika hospitali mbalimbali mkoani Shinyanga
Mdau wa afya,Mzee Sengerema akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati
wa kikao hicho ambapo aliwashukuru wadau wa sekta ya afya kujitokeza kwa
wingi kujadili masuala yanayohusu afya mkoani humo.Angalia Picha Nyingi zaidi <<HAPA>>