HATIMAYE KAMUSOKO ARUDISHWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA
Kiungo
wa Yanga, Thabani Kamusoko ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya
Zimbabwe kinachojiandaa na mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika
dhidi ya Liberia mwezi ujao.
Kocha
Norman Mapeza ameamua kumuita Kamusoko kikosini kwa ajili ya mchezo wao
wa kuwania kufuzu fainali za Afrika baada ya kutoitwa kwa muda mrefu
katika timu hiyo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuitwa kikosini, Kamusoko alisema anamshukuru Mungu baada ya kuchaguliwa kwenye kikosi hicho.
“Kweli
nawashukuru sana watu wote wa Yanga hasa benchi lote la ufundi kwa
namna walivyokuwa wakiniamini na kunipatia nafasi ya kucheza katika
kikosi cha kwanza.
“Naamini
chachu ya mimi kuitwa timu ya taifa inatokana na Yanga na ndiyo maana
leo utaona nimeitwa kwenye timu ya taifa kwa mara nyingine, namshukuru
Kocha Mapeza na wengine wote,” alisema Kamusoko.
Kamusoko anakuwa mchezaji pekee wa Zimbabwe aliyecheza Ligi Kuu Bara msimu uliopita kuitwa katika kikosi cha nchi hiyo.
Baadhi
ya wachezaji walioitwa na Mapeza ambao ni viungo ni Kamusoko, Devon
Chafa (Caps United), Simon Shoko (FC Platinum), Kudakwashe Mahachi (
Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns), Marvelous Nakamba
(Vittese), Danny Phiri (Golden Arrows), Liberty Chakoroma (Ngezi
Platinum), Ovidy Karuru (AmaZulu) na Ronald Chitiyo wa Caps United.