Makubwa Haya: WAFANYAKAZI WA MOCHWARI DAR WATIWA MBARONI KWA KUMWIBIA MAREHEMU KETE ZA ZA DAWA ZA KULEVYA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka
kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za
dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki
dunia akiwa katika nyumba ya wageni.
Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri
kwamba baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red
Carpet' iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na
kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao
wamewauzia ambao nao wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi
"Yule Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye
nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari
Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule
mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa
kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa"
alisema Sirro
Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.
"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo
ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala
lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani
naye amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye
alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally
Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye
alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa
tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro