HII HAPA ORODHA YA NCHI ZENYE WATU WANENE ZAIDI DUNIANI
Mtandao wa CIA’S World Fact umetoa orodha ya nchi zenye idadi kubwa ya
watu wanene duniani ambapo Amerika ya Kaskazini ikiwa na nchi nyingi
zenye idadi kubwa huku Qatar na Kuwait zikiongoza Bara la Asia na Afrika
kukiwa na idadi ndogo ya watu wanene.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya 75% ya watu katika nchi hizi wana
uzito uliopitiliza huku wanawake wakiongoza kwa unene ukilinganisha na
wanaume katika nchi za kiarabu wakati Canada, Marekani na Australia
wanaume wanaongoza kwa zaidi ya 25% dhidi ya wanawake.
Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limesema sababu za nchi hizi kuwa na idadi
kubwa ya watu wanene hazihusiani na Uchumi mkubwa katika nchi hizo bali
upatikanaji wa vyakula visivyokuwa na virutubisho ambavyo wanakula hasa
kutoka viwandani ukilinganisha na nchi za Afrika.