KOCHA WA OMOG KUTUMIA MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP KUKIPANGA KIKOSI CHAKE
Kocha
Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, amepanga kuitumia michuano
ya Kombe la Sportpesa kwa ajili ya kukijenga zaidi kikosi chake kwa
ajili ya msimu ujao.
Simba
ambayo imemaliza msimu huu ikinyakua Kombe la FA huku ikilikosa Kombe
la Ligi Kuu Bara lililotua kwa watani zao wa jadi, Yanga, inatarajiwa
kuwa na mapumziko ya takribani siku tano kabla ya kuanza kujiandaa na
michuano hiyo.
Michuano
hiyo itakayozishirikisha timu nane ambazo ni Simba, Yanga, Singida
United na Jang’ombe Boys kutoka Tanzania na Tusker, Gor Mahia, Nakuru
All Stars na AFC Leopards za Kenya, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
Juni 5, mpaka 11, mwaka huu.
Omog
amesema kuwa: “Tunashukuru tumemaliza msimu salama licha ya kuukosa
ubingwa wa ligi kuu, lakini kitendo cha kuchukua Kombe la FA ni faraja
kubwa kwetu hali ambayo itatufanya msimu ujao tujipange zaidi.
“Baada
ya ligi kumalizika, kinafuata kipindi cha usajili ambapo hatutakiwa
kufanya makosa kwa hilo na hii michuano midogo ambayo tunakwenda
kushiriki, inaweza kutusaidia kuangalia wapi tunatakiwa kujiweka imara
zaidi kabla ya kuanza kwa msimu ujao, lakini pia wale wachezaji
waliokuwa wanakosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, wataanza kuonekana.”