Kiungo
mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amesema kuwa hatakiwi kutupiwa
lawama kwa kushindwa kucheka na nyavu kutokana na ‘ukata’ huo kutomganda
peke yake, kwani hata kinara Simon Msuva wa Yanga, naye ameshindwa
kufunga kwenye mechi zao.
Kichuya,
mwenye mabao 11 kwenye mzunguko huu wa pili, ameifungia timu yake bao
moja tu kwenye mechi 12 mpaka sasa, tofauti na mzunguko wa kwanza ambapo
alifanikiwa kufunga mabao 10 kwenye mechi 15.
Kiungo
huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kushindwa kwake kufunga
kunatokana na ugumu wa ligi ambayo imebakiza mechi tatu ambapo kila timu
inakuwa inacheza kwa tahadhari kuhakikisha kwamba haifungwi.
“Ligi
imekuwa ngumu na tunakutana wakati mgumu hasa kwenye mechi hizi za
mwisho, ndiyo maana unaona spidi yangu ya kufunga imepungua tofauti na
ilivyokuwa awali.
“Lakini
siyo mimi peke yangu ambaye sijafunga hadi sasa, hata Msuva anayewania
tuzo ya ufungaji bora amekomea hapo na mabao yake 12 tofauti na mwanzo,
jambo hilo linaonyesha kwamba kuna ugumu kiasi gani kwenye suala zima la
kucheka na nyavu,” alisema Kichuya.