JTFE YATOA MSAADA KITUO WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA NA WADIAKONIA KKKT -DKMZV.
Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner
Foundation Europe (JTFE) inayojishughulisha na masuala ya watu wenye
Ualbino imetoa msaada wa miwani ya kuzuia mionzi ya jua,viatu, vifaa vya
michezo kwa watoto ikiwemo midoli katika kituo cha kulelea watoto wenye
ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga chenye watoto wenye
ualbino 142,wasioona 26 na wasiosikia 60.
Mbali na kutoa vifaa hivyo katika kituo
cha Buhangija pia JTFE imetoa msaada wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua
na miwani ya kuzuia mionzi ya jua katika Kituo cha Wadiakonia cha Kanisa
la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kilichopo Mwasele
katika manispaa ya Shinyanga.
Akuzungumza jana wakati wa kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa JTFE
yenye makao makuu yake nchini Uholanzi, Pieter Staadegaard alisema
wametoa msaada huo ili kuonesha kuwa wanawajali watoto hao na kwamba wao
ni kama watu wengine katika jamii.
“Huko Uholanzi naishi na watoto watatu kati yao mmoja na
ualbino,nilipowaambia ninakuja Tanzania,wakanipatia zawadi hii ya vifaa
kwa ajili ya watoto ikiwemo hii midoli kwa ajili ya watoto wenzao wa
hapa Buhangija”,alieleza Staadegaard.
Aidha aliitaka jamii kuwathamini na kuwapenda watu wenye ualbino badala
ya kuwafanyia ukatili kwani ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.
Staadegaard alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na
Utetezi JTFE,Josephat Torner na viongozi wa Idara ya wanawake na watoto
na diakonia kutoka kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya
Ushawishi na Utetezi JTFE,Josephat Torner katika kituo cha kulelea
watoto cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akimpa midoli Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi
na Utetezi JTFE,Josephat Torner kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika
kituo cha Buhangija
Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akizungumza wakati wa kupokea zawadi hiyo
Zoezi la kugawa zawadi kwa watoto likiendelea
Watoto wanapokea zawadi.Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake
na Watoto kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria,Edna Shoo
Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akigawa midoli kwa watoto
Watoto wakiwa katika foleni kwa ajili ya zawadi
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi Taasisi ya Kimataifa ya
Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akimvalisha
miwani ya kupunguza mionzi ya jua mmoja wa watoto waliopo katika kituo
cha Buhangija
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akiwa na mtoto mwenye ualbino mara baada ya
kumvalisha miwani
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiwa na mtoto mwenye ualbino
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akimvalisha viatu mtoto mwenye ualbino
Mtoto akivaa viatu,zawadi kutoka JTFE
Watoto wakiendelea kuvaa viatu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
watoto wenye ualbino baada ya kuwapa zawadi ya viatu
Hapa ni katika kituo cha Wadiakonia kanisa la KKKT-DKMZV ,Pichani ni
mkurugenzi wa idara ya wanawake,watoto na diakonia kanisa la KKKT
Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ambarang'u
akimkaribisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner
Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard katika kituo hicho
Mkurugenzi wa idara ya wanawake,watoto na diakonia kanisa la KKKT
Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ambarang'u akielezea
kuhusu kituo hicho ambacho kinalea vijana wa kike wenye ualbino kwa
kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ikiwemo kushona nguo kwa
kutumia cherehani.Wa Kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza katika kituo hicho na kuwataka
vijana hao kuzingatia ujuzi wanaopatiwa ambao utawasaidia katika maisha
yao na waweze kusaidia pia watu wengine
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akimvalisha miwani mmoja wa vijana hao.Wa
kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi Taasisi ya
Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE)Josephat Torner
Vijana hao wakiwa wamevaa miwani ya kupunguza mionzi ya jua
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akigawa mafuta yanayopunguza mionzi ya jua
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiendelea kugawa mafuta
Zoezi la kugawa tisheti zilizotolewa na kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria likiendelea
Mratibu wa Diakonia kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria,Matrida Sanga akimwonesha Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya
Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard kazi
zinazofanywa na vijana hao
Viongozi wa JTFE na vijana wanaolelewa katika nyumba ya wadiakonia
Picha ya pamoja,viongozi wa JTFE,viongozi wa Idara ya wanawake na watoto
na diakonia kutoka kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria na vijana waliopo katika kituo hicho
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog