HIMID MAO SASA MGUU SAWA DENMARK, WAZUNGU WAKO DAR ES SALAAM
kuna
taarifa kuwa, mabosi wa timu ya Randers FC ya Denmark, wapo kwenye
mazungumzo na mabosi wa Azam FC juu ya makubaliano ya kumchukua kiungo
wao, Himid Mao.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Himid kufuzu majaribio ya siku 10 aliyoenda
kuyafanya katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark, mapema
mwezi huu.
Ofisa
Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye
mazungumzo na mabosi hao wa Randers baada ya kuwapa habari kwamba kiungo
wao amefuzu majaribio yake.
“Tupo
kwenye majadiliano na wao, tunasubiri kusikia ofa yao na kama
tukikubaliana basi Himid ataenda kujiunga nao kwa sababu wametuambia
tayari amefuzu, hivyo mazungumzo yaliyopo sasa ni baina yao na sisi,”
alisema Idd.
Naye Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kuwa kama dili hilo litafanikiwa, basi anamtakia kila la heri kiungo wake huyo.
SOURCE: CHAMPIONI