MADRID WALIVYOPOKELEWA MADRID NA MWALI WAO WA LA LIGA
Mabingwa
wa La Liga, Real Madrid wamepokelewa kwa shangwe kubwa jijini Madrid
baada ya rasmi kulibeba kombe hilo katika mechi ya mwisho ya msimu.
Katika
mechi hiyo, Madrid imeitwanga Malaga kwa mabao 2-0 na kujihakikishia
ubingwa dhidi ya Barcelona waliokuwa wakifukuzana nao kwa kasi.
Mashabiki
walijitokeza kwa wingi kuwalaki Madrid wakati wakiwasili katika mitaa
ya jiji la Madrid ambalo ni kubwa zaidi kuliko mengine yote nchini humo.