|
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bungeni
leo kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya Mapato na
matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
|
Na
Raymond Mushumbusi Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa
waajiri na waajiriwa wote nchini kuzingatia Sheria za kazi na kuimarisha
uhusiano katika kazi ili kutumia muda mwingi kufanya kazi badala ya kutatua
migogoro kazini.
Ameyasema
hayo alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na
makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha
2017/2018.
“Niwaombe waajiri na waajiriwa kuzingatia Sheria
za kazi tupunguze migogoro kazini ili tuweze kuendana na azma ya Serikali ya
Awamu ya Tano ya kufanya kazi” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Ameongeza
kuwa Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro ya
kikazi inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa
waajiriwa.
Amezitaja
Sekta zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni
Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.
Katika
kupunguza migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia
uundwaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imeendelea
kutimiza wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika kipindi cha Julai hadi Februari 2016 jumla ya migogoro 8,832 ilisajiliwa na
kati ya hiyo migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya migogoro iliyosajiliwa
imesuluhishwa.